Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vipodozi Vyenye Kemikali Changamoto Kwa Wanawake

Kemiko.jpeg COSTECH kuendeleza tafiti mbalimbali

Wed, 13 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya watafiti na wabunifu nchini wameitaka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)kujiwekeza katika kujenga viwanda vidogo vidogo vitakavyo wasaidia wabunifu na watafiti kupeleka bidhaa zao.

Hayo yamesemwa na Mtafiti wa mimea na vipodozi Salvatore Lugangila wakati alipokuwa na mahojiano maalumu.

Amesema kuwa COSTECH ina uwezo mkubwa wa kutafuta wafadhili wakubwa watakaosaidia tume hiyo katika ujenzi wa viwanda vitakavyokuwa vina wakutanisha watafiti na wabunifu kuonyesha bunifu zao.

"Serikali inatakiwa iangalie COSTECH kwa kuiwezesha kifedha kama vile wanavyo thamini maji, na hivyo hivyo wathamini tume hiyo ambayo inalinda afya za watu kwa kufanya tafiti mbalimbali na kusaidia afya za Watanzania hasa wanaotumia kemikali "Alisema

Aidha pamoja na mambo mengine amesema watu wengi huko mitaani wanadanganyana kuhusu vipodozi na kujikuta wakichukua vipodozi feki vinavyo changanywa na kemikali ya kufanya ngozi kuwa nyeupe bila kujali madhara yake.

Amefafanua kuwa mimea inayotokana na tafiti walizofanya ni salama na kwamba kazi yake kubwa ni kutibu ngozi iliyoathirika kwa kemikali na kurudi kuwa katika hali yake ya Kawaida.

Amesema yapo maeneo ambayo yameathirika kwa matumizi ya vipodozi vikali ikiwemo maeneo ya majiji yenye watu wengi mchanganyiko na kuitaka jamii kuacha kukimbilia kutaka weupe wa haraka na badala yake watumie watafiti walio chini ya COSTECH ili kupata bidhaa iliyokidhi viwango.

Lugangila anasema katika tafiti walizofanya waliweza kugundua mambo mbalimbali ikiwemo sababu za wanawake kutumia vipodozi vyenye kemikali na kuwa weupe ni kutokana na wanaume kupenda wanawake weupe tofauti na wanawake weusi.

"Unakuta dada zetu wanakimbilia kwenye vipodozi vikali ili waweze kuwa weupe wawavutie wanaume bila kujali kuwa bidhaa wanayotumia inaathari kubwa katika ngozi zao hapo baadae" Alisema Lugangila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live