Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana waongoza maambukizi VVU asilimia 50

Hivleo Ed Vijana waongoza maambukizi VVU asilimia 50

Tue, 22 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) imesema asilimia 50 ya maambukizi mapya wanapata vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 29.

Tacaids imebainisha hayo leo Jumanne Februari 22, 2022 katika hafla ya kusaini makubaliano ya ushiriki wa pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi.

Mkurugenzi mkuu wa Tacaids, Dk Leonard Maboko amesema makubaliano hayo yanafanyika wakati nchi bado ina kazi kubwa ya kufanya kutokomeza ugonjwa huo huku changamoto kubwa akiitaja kuwa ni maambukizi mapya miongoni mwa vijana.

“Maambukizi mapya yanatokea zaidi kwa vijana kati ya miaka 15 hadi 29, wanachangia asilimia 50 ya maambukizi mapya, hiki ni kizazi cha kesho hivyo tuna kazi kubwa ya kufanya kupunguza maambukizi mapya miongoni mwao lazima tulipe kundi hili kipaumbele,” amesema.

Amesema bado elimu inahitajika kwa ukubwa zaidi watu waelimike, “Tuwaweke wazi waache ngono kama hawezi atumie kinga na yule aliyepo kwenye ndoa akae na mwenzi wake inaonekana bado kuna kazi.”

Dk Maboko amesema nchi inategemea fedha nyingi kutoka kwa wafadhili.

“Asilimia 94 ya fedha za kupambana na ukimwi tunapata kwa wafadhili wa nje ni asilimia 4 pekee tunaipata ndani. Ipo siku watasema wamechoka, kifupi hatutakua na wafadhili bado tunatakiwa kuendelea kupambana tufikie 0 maambukizi mapya,” amesema.

Mkurugenzi wa idara ya huduma za wanachama TPST, Zachy Mbenna amesema ushirikiano baina yao na Tacaids utasaidia kwa kuwa mfano bora kwenye kampuni ndogo na za kati kushiriki pamoja kutokomeza ugonjwa huo nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live