Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana waathirika wakubwa, 60% hawajui UKIWMI unaeneaje

D54cac7974345d2beebea0b46902b1b2 Vijana waathirika wakubwa, 60% hawajui UKIWMI unaeneaje

Sat, 11 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKURUGENZI wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, amesema Vijana ni kundi lililoathiriwa zaidi na maambukizi ya UKIMWI ambapo watu 200 hupata maambukizi mapya kwa siku nchini.

"Asilimia 40 ya maambukizi mapya yanatokea kwa vijana wa miaka 15 hadi 24, kuna taarifa tulizitoa kwamba watu 200 kila siku wanapata maambukizi ya Ukimwi, maana yake vijana 80 walikuwa wanapata maambukizi kila siku," amesema Dk Maboko na kuongeza

"Ukiwauliza vijana hao wa miaka 15-24 elimu kuhusu Ukimwi unavyoenea na jinsi ya kuzuia chini asilimia 40 ndiyo walikuwa wanajua lakini ile asilimia 60 ya vijana hawajui yaani unamuuliza Ukimwi unaeneaje hajui yupo tu." amesema

Chanzo: www.habarileo.co.tz