Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo 27,429 vimeripotiwa kutokana na UKIMWI

HIVandAIDSbasics Takwimu hizi ni za mwaka 2019

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa takriban watu wazima na watoto 77,084 wamepata maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi katika kipindi cha mwaka 2019 huku vifo vikiwa ni 27,429.

Hayo yamejiri jijini Dar es salaam katika warsha ya wanahabari nchini ambayo imeratibiwa na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi nchini –TACAIDS kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto ya VVU na Ukimwi kupitia mfuko wa udhamini wa kudhibiti ugonjwa huo (ATF).

Akizungumza wakati akifungua warsha hiyo,Kaimu Mkurugenzi wa TACAIDS Jummane Isango amesema kuanzishwa kwa mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi utasaidia kukusanya rasilimali za ndani na kupunguza utegemezi kutoka wa wahisani wa nje kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwemo Dawa za ARVs.

‘Rasilimali hizi ambazo tunategemea kwa wenzetu kwa kiasi kikubwa karibia asilimia 90 zinaenda zikiwa zikiwa zinapungua na huu utgemezi pamoja na wadau wenyewe wanatushauri tushitukie kwani misaada itakapoisha itakuwa ni shida hivyo ndo maana tukaja na wazo la kuwa na mfuko wa Udhamini wa kudhibi Ukimwi kama nchi utakao tusaidia kukusanya rasilimali za ndani’amesema Isango

Akiwasilisha mada ya Hali ya Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania Meneja wa Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi Peter Kivugo amesema licha ya kushamiri maambukizi ya VVU katika baadhi ya mikoa na tangu Mpango wa Taifa wa Tiba za UKIMWI uanze mwaka 2004, WAVIU wanaopata huduma za tiba wameendelea kuongezeka.

‘Kampeni na huduma za kupima maambukizi ya VVU zimeendelea kuboreka nchini Kwa mwaka 2019, zaidi ya watu milioni 10 walipata huduma ya kupima VVU.Miongini mwa waliopima, watu 237,708 walibainika kuwa na maambukizi Kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita zaidi ya watu laki 2 wamekuwa wakigundulika kuwa na maambukizi ya VVU kwa siku’amesem Kivugo

Aidha ameyataja mafanikio kuwa ni pamoja na 92% ya WAVIU walioko kwenye huduma za tiba na matunzo wafebuza VVU kutoka 88%, Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kwa 98% na Kuongezeka kwa WAVIU waliounganishwa na huduma za Tiba na matunzo kutoka 91% -98%.

Kwa upande wao baadhi ya wanahabari akiwemo Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Herieth Makweta pamoja Mratibu wa Jukwaa la wanawake wanoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania Veronica Lyimo wamesema wameongeza uelewa wa namna ya wadau balimbali hasa wafanyabiashara wanapaswa kuchagia mfuko huo.

Kwenye warsha hiyo pia ameshiriki Meneja wa Elimu ya Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania –TRA Julius Mjenga amesema Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi utakuwa na faida kwani wafanyabiashara watakapotoa mchango watapunguziwa mzigo wa kodi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live