Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viagra ya wanawake kuingia sokoni Septemba

65321 Pic+viagra

Wed, 3 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Washington. Shirika linalohusika na udhibiti wa chakula na dawa nchini Marekani (FDA), hivi majuzi liliidhinisha dawa mpya kutibu tatizo la ukosefu wa hisia za kingono miongoni mwa wanawake ambao hawajafikia ukomo wa hedhi.

Ukosefu wa hisia hizo husababishwa na mwanamke kutoshiriki katika vitendo vinavyoweza kuvutia hisia za ngono bila ya kuhisishwa na tatizo lolote.

Kemikali kwa jina Vyleese imejaribiwa kutengeneza kile ambacho kinaweza kuitwa Viagra ya kike.

Hili ni swala tata , kwa kuwa baadhi ya wataalam wanahoji asili ya tatizo la hisia za kingono na kukosoa ukosefu wa msisimko wa mapema wakati mwathirika anapotumia.

Viagra hiyo imetengenezwa na kampuni ya Teknolojia ya Palatin Technologies na kuruhusiwa kuuzwa na Amag Pharmaceuticals.

Viagra hiyo mpya hutumika kupitia sindano ambayo husisimua njia ya akili inayotumika katika hisia za ngono itaanza kupatikana katika baadhi ya maduka ya dawa kuanzia Septemba.

Pia Soma

Ikilinganishwa na dawa nyingine, dawa hiyo haifanyi kazi katika mfumo wa mishipa, lakini huongeza hamu ya tendo la ngono katika mfumo wa neva.

Vyleesi itashindana na Addyi ya watengenezaji dawa wa Sprout, dawa ya kila siku ambapo iliidhinishwa 2015 na kwamba watumiaji hawafai kutumia pombe wakati wanapoitumia.

Chanzo: mwananchi.co.tz