Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIJANA WANAONGOZA KUPATA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

7190ee389e0bdc3a5d5118dd2286a3c8 VIJANA WANAONGOZA KUPATA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Mon, 8 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TUME ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) imesema maambukizi mapya mengi yanayogundulika ni kundi la vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 24.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dk Leonard Maboko akiwasilisha ripoti ya hali ya maambukizi ya ukimwi kitaifa na kimataifa kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Dawa za Kulevya amesema hali ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi hapa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa kwa mwaka 2019.

Amesema watu wazima kuanzia miaka 15 ni takribani 68,484 kati yao wanawake 39, 614, wanaume 28,870 na Watoto chini ya miaka 15 ni 8600 jumla yake ikiwa ni 77, 084.

Licha ya takwimu kupungua lakini ripoti imeoyesha katika maambukizi mapya yanayoripotiwa ni kundi la vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 na maambukizi yamefikia asilimia 40 na kati ya hao kundi linaloathirika zaidi ni kundi la vijana wa kike kwa asilimia 80.

Chanzo: habarileo.co.tz