Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Zimamoto zatumika kupulizia dawa Kariakoo

VIDEO: Zimamoto zatumika kupulizia dawa Kariakoo

Sat, 28 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Zoezi la upulizaji dawa kwaajili ya kuuwa vimelea mbalimbali vya magojwa kwa kutumia magari ya kikosi cha zimamoto limeanza katika eneo la kariakoo jijini Dar es Salaam.

Machi 24 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliagiza kupulizwa dawa katika maeneo mbalimbali ili kuua vimelea vya magonjwa ikiwemo virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mapafu (Covid-19)

Akizungumza leo Ijumaa Machi 27 mratibu wa udhibiti wa ugonjwa wa malaria mkoa, Dk Ford Sogela amesema wameanza kutekeleza zoezi hilo kwa kuyapa kipaumbele maeneo yenye mkusanyiko wa watu ikiwemo kwenye vituo vya mabasi na kwenye masoko.

“Zoezi hili tumeanza kwa kuangalia maeneo yenye mkusanyiko wa watu kama vituo vya mabasi, mwendokasi, masoko na kwenye hoteli ambazo hupokea raia wa kigeni,” amesema Dk Songela.

Pia amesema zoezi hilo litakuwa likitekelezwa nyakati za usiku kwa kuwa maeneo mengi ni ya biashara ili watakaporejea asubuhi wakute kazi imeshafanyika na kuepuka usumbufu.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Rashid Mfaume amesema zoezi hilo lilianzia katika vituo vya mwendokasi, stendi za mabasi na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kinondoni.

Pia Soma

Advertisement
Amesema dawa ya maji inayopuliziwa na gari la zimamoto ni dawa ya kawaida ambayo hutumika hata kwenye maji ya kunywa na kuwatoa hofu wananchi kwa kuwa zoezi hilo linalenga kuwaweka salama.

“Hii dawa tunapulizia wadudu wanaotambaa mfano mbu leo tunazungumzia corona lakini kuna wadudu wengine mfano mbu, Dar es salaam imekuwa ikikumbwa na dengue,” amesema Dk Mfaume.

Chanzo: mwananchi.co.tz