Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Viongozi wamiminika Muhimbili kumjulia hali Kigwangalla

Sun, 5 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mawaziri mbalimbali wamefika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla aliyepata ajali leo asubuhi Jumamosi Agosti 4, 2018.

Dk Kigwangalla amepata ajali eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini.

Awali,  waziri huyo alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta na kisha Muhimbili.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alikuwa wa kwanza kufika hospitalini hapo na kufuatiwa na naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dk Ashatu Kijaji na naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni aliwasili na  viongozi mbalimbali wizara hiyo na ya Maliasili na Utalii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya na mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru pamoja na jopo  la madaktari walimpokea Dk Kigwangalla katika kitengo cha magonjwa ya dharura Muhimbili.

Ndugu, jamaa na marafiki pia walifika hospitalini hapo kumjulia hali waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa Nzega Vijijini.

Chanzo: mwananchi.co.tz