Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Serikali yatoa utaratibu wa uvaaji maski kujikinga na corona

99562 Maskipic VIDEO: Serikali yatoa utaratibu wa uvaaji maski kujikinga na corona

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa uvaaji wa maski bila kufuata utaratibu maalumu ni hatari kwa afya kwani inaweza kukuletea maambukizi ya magonjwa. Maski huvaliwa kwa mtu aliyeambukizwa ili asiambukize wengine na inatakiwa kuvaliwa kila baada ya masaa manne na kubadilishwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 18, 2020, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa ya mlipuko, Dk Janeth Mghaba ameshauri kuwa watu wazingatie matumizi sahihi ya uvaaji wa maski “Maski inavaliwa na mtu ambaye tayari ana maambukizi, ili asiwaambukize wengine, tunasema kwamba ukisikia unadalili za kukohoa basi wewe vaa maski yako nenda kwenye kituo cha karibu cha hospitali," amesema Dk Mghaba. Amefafanua zaidi kuwa maski zinatakiwa kuvaliwa sehemu zenye msongamano au watu wengi, hivyo kwa kuwa Serikali imekataza misongamano hatotegemea kumuona mtu ambaye ni mzima amevaa maski akipita sehemu ambazo hazina msongamano.

Chanzo: mwananchi.co.tz