Dar es Salaam. Isabela Mwampamba ambaye ni Mtanzania wa kwanza kupata maambukizi ya virusi vya corona nchini awaomba msamaha Watanzania.
Ameomba radhi kwa madai kuwa yeye anajiona kama chanzo cha kuingia kwa ugonjwa huo nchini.
Akizungumza leo Jumatano Machi 18, 2020 kwa njia ya simu katika mkutano wa wanahabari ulioandaliwa na Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu uliofanyika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema,
“ninaendelea vizuri, namshukuru Mungu kwa kunilinda nawaomba msahama watanzania kwa maana kuwa mgonjwa wa kwanza kuugua corona iliyoleta taharuki nchi nzima na watu wengi wanaona kwamba mimi ni kisababishi."
"Niko hapa nikiomba msamaha, naamini kuwa Mungu ataendelea kutuponya.”
Isabela amesema kwa sasa hana dalili zozote za ugonjwa huo na kwamba hana homa wala mafua.
Habari zinazohusiana na hii
- MPYA: Mgonjwa wa corona agundulika nchini Tanzania
- Jinsi mgonjwa wa corona alivyoingia Tanzania hadi akagundulika
- Watafiti Uganda wagundua virusi vya corona kwenye mwili wa ngamia na popo
- Waziri aeleza nini kifanyike kuhusu corona