Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: MSD yafukuzia kupewa jukumu kununua dawa kwa nchi za Sadc

Thu, 21 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Bohari Kuu ya Dawa (MSD) itapewa jukumu la kununua dawa kwa ajili ya nchi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) iwapo mwongozo wa huduma ya ununuzi wa dawa wa pamoja (SPPS) utakubaliwa na kupitishwa na wataalamu kutoka nchi 16 za jumuiya hiyo.

Mkutano wa wataalamu kutoka nchi wanachama wa Sadc umefanyika leo Alhamisi Machi 21, 2019 jijini Dar es Salaam kujadili mwongozo wa huduma ya ununuzi wa pamoja wa dawa ambao ulipitishwa na mawaziri wa afya tangu mwaka 2017.

Akizungumzia mkutano huo, mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi, amesema jukumu hilo litakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania ikiwamo kupunguza gharama za dawa na MSD kulipwa gharama za uendeshaji na nchi wanachama.

“Mpango huu utakuwa na manufaa kwetu Watanzania,  kwanza utatoa nafasi kwa viwanda vyetu vya ndani na pili  Tanzania itakuwa ni kiungo na nchi nyingine hasa katika ku-supply dawa,” amesema Msasi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ununuzi wa MSD Abdul Mwanja, amesema bohari hiyo ilishindanishwa na chi nyingine na kuonekana ina uwezo na uzoefu zaidi kutokana na kutekeleza ununuzi wa pamoja wa dawa nchini.

Amesema wamejipanga kikamilifu kubeba jukumu hilo kwa sababu wana uzoefu wa kutosha katika ununuzi wa dawa wa pamoja ndani ya nchi.

Amebainisha kuwa tayari MSD imeanzisha ofisi maalumu itakayoshughulika na ununuzi wa dawa kwa nchi za Sadc.

“Sisi tuna advantage kubwa, mpaka sasa tuna wazalishaji wa dawa 108 wanaoiuzia dawa MSD na tangu tulipoanza kununua kwa pamoja tumepunguza bei kwa zaidi ya asilimia 40. Kwa hiyo tukianza kununua kwa pamoja kama Sadc, tutaendelea kupunguza bei,” amesema Mwanja.

Ofisa programu mwandamizi wa afya na lishe kutoka Sadc, Willy Hamis amesema viwanda vya dawa vilivyopo katika ukanda wa Sadc vitapewa kipaumbele kununua dawa ili kukuza soko la ndani.

Amesema manufaa ya SPPS ni kuongeza ushindani katika uzalishaji wa dawa, kuongeza uwazi katika ununuzi, kuweka viwango vya ubora vinavyofanana na kuhifadhi kumbukumbu za wataalamu wa dawa.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz