Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Afya ya Kigwangalla yazidi kuimarika, atakiwa kupumzika

Video Archive
Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Afya ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla inaeendelea kuimarika na madaktari wameelekeza apate muda mwingi wa kupumzika.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Agosti 6, 2018 na naibu Waziri wa wizara hiyo, Japhet Hasunga muda mfupi baada ya kutoka wodini kumjulia hali Kigwangalla.

Waziri huyo alipata ajali Agosti 4, 2018 mkoani Manyara na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Selian jijini Arusha na siku hiyo hiyo kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Akizungumza na MCL Digital, Hasunga amesema madaktari wamefanikiwa kurudisha kila kitu katika hali ya kawaida na kwa sasa wanafuatilia maumivu madogomadogo.

“Ameshakuwa kawaida anazungumza vizuri ninaweza kusema hali yake imeimarika ila bado wanafuatilia maeneo ambayo ana maumivu,” amesema Hasunga.

Amesema taratibu nyingine za kitabibu zitaendelea baada ya uvimbe alionao kupungua.

Soma Zaidi:

VIDEO: Kigwangalla: Nipo salama, nawashukuru Watanzania

Hasunga amesema jopo la madaktari linalomtibu Dk Kigwangalla limehauri  apate muda mwingi wa kupumzika hivyo hatarajiwi kupata wageni.

"Tunawaomba watu wanaotamani kumjulia hali waendelee kumuombea wakiwa huko huko tutawapa taarifa za maendeleo ya afya yake," amesema.

Kuhusu uwekezano wa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi,  Hasunga amesema hakuna mpango huo.

“Tunaamini atatibiwa hapa na kupona. Huduma zinazotolewa hapa ni bora zaidi na yeye mwenyewe anaridhishwa ingekuwa tofauti na hapo angesema kwa kuwa yeye ni daktari," amesema.

Ofisa uhusiano wa MNH, John Stephen amesema madaktari wanaendelea kumpatia matibabu kulingana na vipimo vilivyofanywa na hospitali hiyo.

“Inawezekana mgonjwa akaja na majibu kutoka hospitali nyingine ila utaratibu wetu hapa lazima madaktari wa hapa wafanye vipimo ndio matibabu yaendelee na hilo limefanyika," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz