Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uyoga wenye kemikali za kulevya wahalalishwa

56541 UYOGAPIC

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Los Angeles, Marekani. Jiji la Denver jana Jumatano lilikuwa la kwanza kuhalalisha matumizi ya uyoga unaolevya (psychedelic mushrooms), baada ya wapigakura kupitisha kwa kupata ushindi wa tofauti ndogo sheria inayolegeza masharti ya matumizi ya mmea huo.

Sheria mpya imelegeza masharti ya matumizi na umiliki wa mmea huo, ambao pia hujulikana kama uyoga wa miujiza, kwa watu wenye umri kuanzia miaka 21.

Sheria mpya, hata hivyo, haihalalishi kununua uyoga huo, kuuza au kumiliki. Inaelekeza maofisa wa polisi kutowachukulia watumiaji wa uyoga huo kama kipaumbele katika majukumu yao.

Ingawa jitihada za kampeni ya kutaka uyoga huo uhalalishwe zilionekana kuelekea kugonga mwamba, Jumatano alasiri hali ilibadilika baada ya taasisi ya Initiative 301 kuonekana kuelekea kupata ushindi wa karibu asilimia 50.6 ya kura.

Kinara wa kampeni za kutaka mmea huo uhalishwe, Kevin matthews alisema saa 21 na nusu za kura hizo zilikuwa ngumu wakati alipohojiwa na gazeti la The Denver Post baada ya matokeo ya kura kutangazwa.

"Kama mambo yataendelea hivi, itakuwa ni kinyume cha matazamio. Hivi ndivyo inavyotokea wakati timu ndogo ya watu wanaojituma inapoungana chini ya wazo moja la kufanya mabadiliko," alisema Matthews.

Viongozi walisema kura hizo zitaidhinishwa Mei 16 baada ya kura zote za jeshini na watu walio nje ya jimbo zitakapohesabiwa.

Wanaounga mkono sheria hiyo mpya wanasema kemikali asili aina ya psilocybin iliyo katika uyoga huo haichukuliwi kama inalevya na inaweza kutumiwa kukabiliana na msongo au maumivu sugu (opioid), mambo ambayo husababisha maelfu ya vifo nchini Marekani.

"Binadamu wametumia uyoga huu kwa maelfu ya miaka kwa ajili ya matibabu, utamaduni na masuala ya kiimani," iloisema taasisi ya Decriminalize Denver, inayoongozwa na Matthews na ambayo mwezi Januari ilitangaza kuwa imekusanya saini za kutosha ili suala hilo lipigiwe kura.

Kupitishwa kwa sheria hiyo, kwa mara nyingine, kumelifanya jimbo la Colorado kuongoza katika kuhalalisha dawa za kulevya baada ya kuwa moja ya majimbo yaliyohalalisha bangi mwaka 2012.

"Denver inabadilika haraka kuwa jiji la dawa haramu duniani. Ukweli ni kwamba hatujui ni kwa muda gani athari za dawa hizi



Chanzo: mwananchi.co.tz