Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uvivu watajwa chanzo cha saratani, kisukari

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Washington, Marekani. Ripoti ya Shirika la Afya Duniani  (WHO) imesema mtu mmoja kati ya watu wazima wanne duniani anakabiliwa na hatari ya kupata magonjwa ya kisukari na saratani kwa sababu ya kutofanya mazoezi ya kutosha.

Jumla ya watu bilioni 1.4 hawafikii kiwango kilichokubaliwa na shirika hilo cha kufanya mazoezi, kinachowataka watu kufanya shughuli za wastani kwa angalau dakika 150 au dakika 75 za mazoezi ya kazi zenye nguvu kwa wiki.

Kwa mujibu wa taarifa za WHO, asilimia 27.5 ya watu wazima duniani walifanya mazoezi ya kutosha kwa mwaka 2016, idadi iliyoshuka kwa asilimia moja tangu mwaka 2001.

Mataifa yanayofanya vibaya zaidi ni pamoja na Kuwait, Saudi Arabia na Iraq. Uganda na Msumbiji zina idadi ndogo zaidi ya watu wasiofanya mazoezi ya kutosha zikiwa na asilimia sita tu.

WHO inasema katika mataifa yenye utajiri, watu wanazidi kutokuwa na afya nzuri kwa sababu wanatumia kazi zao na muda wao wa mapumziko wakikaa badala ya kutembea na kwa kutumia magari sana.

Shirika hilo linasema watu wanaopata kiwango kidogo cha mshahara katika mataifa yenye kipato kidogo, ni asilimia 16 ambao hawafanyi mazoezi. Katika mataifa yenye pato la wastani ni asilimia 28 na mataifa yenye pato kubwa ni asilimia 37. Kwa hivyo ni wazi kwamba mataifa yenye utajiri yana watu wengi wasiofanya mazoezi.´

WHO imelitaja China kuwa mfano bora, ambapo idadi ya raia wanaofanya mazoezi ya nje imeongezeka tangu mwaka 2001.

Imesema tu watu kufanya mazoezi na badala yake ni Serikali lazima ihakikishe miundombinu ipo na inachangia kuongezeka kwa watu wanaotembea kwa miguu na wanaotumia baiskeli kama chombo cha usafiri, pamoja na wanaoshiriki michezo na burudani.

WHO imesema wakati mataifa mengi yakiwa na mipango ya kukabili tatizo la watu kutokufanya mazoezi, ni machache ambayo yametekeleza mipango hiyo katika njia yenye manufaa.

Ripoti hiyo iliyochapishwa kwenye jarida la afya la The Lancet, imetokana na utafiti uliofanywa miongoni mwa mwa watu milioni 1.9 katika mataifa 168.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz