Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uviko-19 yaua watu milioni 15

Coronavirus?fit=1600%2C900&ssl=1 Uviko-19 yaua watu milioni 15

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema watu milioni 15 wamefariki dunia kutokana na janga la corona katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari mwaka 2020 hadi Disemba mwaka 2021 katika maeneo mbalimbali duniani.

Kwa mujibu wa taarifa mpya ya WHO kuhusu janga la corona, idadi hiyo ni mara tatu zaidi ya idadi ambayo ilikadiriwa hapo awali katika takwimu za shirika hilo.

WHO imesema vifo vingi vya watu hao vimetokea nchini India ambapo watu milioni 4.7 wameripotiwa kufariki dunia kutokana na corona katika kipindi hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuna umuhimu kwa mataifa kuongeza nguvu katika kukabiliana na janga la corona hasa kudhibiti maambulizi ya virusi vya ugonjwa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live