Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utumiaji vyandarua uko chini asilimia 59

CHANDA Utumiaji vyandarua uko chini asilimia 59

Sun, 12 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UTUMIAJI wa vyandarua Zanzibar upo chini kwa asilimia 59, hali inayochangia kuongezeka kwa maradhi ya malaria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Tathmini wa Ufuatiliaji Kitengo cha Kumaliza Malaria Zanzibar, Mohammed Haji Ali, alisema watu 8,869 wameugua ugonjwa wa malaria visiwani Zanzibar kuanzia Januari hadi Juni, mwaka huu.

Alisema kati ya wagonjwa hao, 5,500 waliripotiwa kuanzia Januari hadi Machi na wengine 3,369 waliripotiwa kuanzia Aprili hadi Juni.

Alisema kuwa Oktoba hadi Desemba mwaka jana, Zanzibar iliripoti wagonjwa wa malaria 3,635.

Ofisa huyo alisema ongezeko la wagonjwa hao limesababishwa na kuwapo mazalia mengi ya mbu yaliyochangiwa na mvua ya masika iliyomalizika hivi karibuni.

Alisema endapo wananchi watatumia vyandarua kwa usahihi, ugonjwa huo utaondoka kabisa.

Alisema kitengo hicho tayari kimeanza kuchukua hatua za tahadhari kwa kuwakinga wananchi ikiwamo kupanga mikakati ya kunusuru jamii kuambukizwa zaidi.

Alitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuelimisha jamii kujilinda na ugonjwa huo, kuwapima wananchi ambao katika maeneo yao kuna maambukizi mengi, kugawa vyandarua kwa wananchi wote katika shehia na kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya kinga ya malaria.

Aliitaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na kufuatilia wagonjwa wa malaria majumbani baada ya kupata ripoti kutoka hospitali na vituo vya afya.

Ofisa huyo alitoa wito kwa wananchi kubadilika kwa kutumia vyandarua kujikinga na malaria kwa sababu ugonjwa huo bado upo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live