Serikali imetenga shilingi bilioni 5 katika mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambapo kati ya fedha hizo, shilingi milioni 224.7 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la huduma ya usafishaji damu.
Kauli hiyo imebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel leo Jijini Dodoma wakati akijibu maswali bungeni na kueleza kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa, matatizo yatokanayo na utoaji mimba ni moja ya sababu zinazochangia vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 10%.
Hata hivyo, amesema madhara yanayotokana na utoaji wa mimba usio salama ni pamoja na uambukizo mkali wa mfumo wa uzazi (Septic Abortion) ambao unaweza kupelekea mgonjwa kutolewa mfuko wa uzazi na wakati mwingine kupoteza maisha.