Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti wa viashiria vya Ukimwi kuwekwa wazi Desemba

Ukimwi Pic Data Utafiti wa viashiria vya Ukimwi kuwekwa wazi Desemba

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matokeo ya utafiti wa viashiria na Matokeo ya Ukimwi Tanzania (THIS) ya mwaka 2022/23 yatawekwa hadharani Desemba Mosi mwaka huu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani.

Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Jenista Mhagama ameyasema hayo leo, Jumanne Oktoba 31, 2023 wakati akielezea kukakamilika kwa utafiti huo.

“Hatua iliyofikiwa sasa ni kuweka data na taarifa katika utaratibu unaotakiwa. Tunatarajia utafiti huo kwa ujumla wake na matokeo yake na data zake zote uzinduliwe rasmi Desemba Mosi mwaka 2023 katika maadhimisho ya Ukimwi duniani,”amesema.

New Content Item (1)

Amesema taarifa ya awali inaonyesha kwamba Tanzania imepata matokeo chanya katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kwa idadi ya maambukizi mapya kuendelea kupungua ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2016/17.

Mhagama amewataka Watanzania kujiandaa kupokea taarifa kamili ya utafiti huo Desemba Mosi mwaka huu.

Amesema lengo la tafiti hizo zinazofanyika kila baada ya miaka mitano nchini ni kupima matokeo ya juhudi za Taifa katika kuhakikisha wanafanya mapambano dhabiti dhidi ya Ukimwi.

Kwa upande wake, Mkazi wa Kikuyu Robert Raphael amewataka vijana wasibweteke na matokeo hayo ya awali bali waendelee na jitihada za kujikinga na ugonjwa huo.

Utafiti huo umefanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar (OSGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Zanzibar (Zac).

Wengine ni Wizara ya Afya kwa usaidizi wa kitaalam kutoka Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC), Chuo Kikuu cha Colombia Marekani (ICAP) kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani chini ya Mfuko wa rais wa Dharura wa Kupambana na Ukimwi (PEPFAR).

Matokeo ya utafiti kama huo wa mwaka 2016/17 yalionyesha maambukizi mapya ya VVU kwa mwaka kwa watu wenye umri wa miaka 15-64 nchini ni asilimia 0.25 (kwa wanawake ni asilimia 0.34 na wanaume ni asilimia 0.17).

Takwimu hizo zikimaanisha kuwa maambukizi mapya kwa watu wenye umri kati ya miaka 15-64 nchini Tanzania ni takribani watu 72,000 kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live