Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti wa Kisayansi: Boksa pana zinaongeza nguvu za kiume

Boksa Nm Utafiti wa Kisayansi: Boksa pana zinaongeza nguvu za kiume

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tafiti za kisayansi za masuala ya uzazi zimebaini kuwa, nguo za ndani hasa zinazobana kwa wanaume na zile za aina ya nailoni (nylon) zinaathiri uwezo wa mbegu za kiume, hivyo kushindwa kutunga mimba.

Utafiti huo umeofanywa katika nchi za Ufaransa na Uingereza na kuchapishwa katika Gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza unabainisha kuwa, wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana na zile zinazotengezwa kwa malighafi ya nailoni, mbegu zao za kiume (manii) huwa nyepesi na kupoteza uwezo wa kutunga mimba.

Vazi la ndani la wanaume linalojulikana kama boksa na nguo nyingine za ndani za kubana zenye asili ya nailoni, zinakuwa na athari kubwa zaidi hasa zinapovaliwa katika sehemu zenye joto, kama vile jijini Dar es Salaam.

Kutokana na matokeo hayo, wanasayansi wameonya kuwa wanaume wanapaswa kuchukua tahadhari, hasa kutokana na tafiti nyingi za karibuni kuthibitisha kuongezeka kwa matatizo ya mbegu za kukosa uwezo wa kutunga mimbao katika nyumba ya uzazi ya mwanamke

Akizungumzia utafiti huo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, amesema kuwa, upo ukweli kutokana na mbegu za kiume kuwa nje ya mwili wa mwanamume tofauti na mwanamke ambaye kizazi chake kipo ndani.

Amesema kuwa, kwa kawaida mwanamume anayeishi maeneo ya joto anapaswa kuwa makini sana, ili kuhifadhi vizuri manii yake anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa.

Aidha, tafiti hizo zinaeleza kuwa kuvaa nguo za ndani zilizo pana kunaweza kuwa njia rahisi kwa wanaume kuimarisha mbegu za kiume na homoni zinazozidhibiti, utafiti uliofanyika nchini Marekani umeeleza.

Utafiti uliowahusisha wanaume 656, uliofanywa na Chuo cha Afya cha Havard TH Chan nchini Marekani, unaeleza kwamba, wanaovaa boxer zilizo kubwa walikuwa na ongezeko kwa 25% ya ubora wa mbegu za kiume kuliko wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana. Wataalamu wanasema mtindo huu rahisi wa maisha unaweza kuboresha uzazi wa wanaume.

Kutokuwepo kwa hali ya joto kwenye maungo ya kiume kunaweza kuwa sababu ya kupunguza ubora wa mbegu za kiume. Uzalishaji wa mbegu za kiume haupendelei joto la zaidi ya nyuzi 34C, ndio maana korodani huning'nia kando ya mwili.

Watafiti wamebaini kuwa wanaume wanaokwenda hospitali kwa ajili ya masuala ya uzazi wakiwa wamevaa nguo za ndani zisizobana wanakuwa ongezeko la ubora wa mbegu za kwa 17%. Hata hivyo, maumbo ya mbegu hizo haziathiriwi wala ubora wa vinasaba vyake.

Pia watafiti walizingatia vitu kadha wa kadha ambavyo vinaweza kuathiri mbegu za kiume ikiwemo, Umri, uzito wa mwili na tabia kama kuvuta sigara, mazoea ya kutumia maji ya moto kwenye mabeseni ya kuogea vyote vinakisiwa kuwa joto lake linaweza kuwa chanzo cha tatizo.

Utafiti umebaini kuwa homoni zilizo kwenye ubongo zenye kazi ya kuziambia korodani kutengeneza mbegu za kiume, huitwa follicle stimulating hormone zilikuwa chini kwa 14% kwa wale wanaovaa nguo za ndani zisizobana.

Katika nchi za Ufaransa na Uingereza ambako utafiti huo umeafanywa umebaini kuwa, nchini Ufaransa upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi umeanza kutokea tangu mwanzoni mwa 1990 ambapo hapo awali iliaminika kuwa, kupungua kwa uwezo wa mbegu za kiume kulitokana na sababu kama vile mtindo wa maisha, ulaji na matumizi ya dawa kupindukia na matumizi ya vyakula vyenye kemikali nyingi, lakini safari hii utafiti umebaini kuwa matumizi ya nguo za ndani yamekuwa yakiwaathiri wanaume wengi.

Mtafiti wa Uingereza, Profesa Richard Sharpe kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh anasema kuwa, tatizo hilo linaweza kuepukwa ikiwa mhusika atajitahidi kuvaa nguo zinazokubalika na mahala alipo. Hata hivyo, anapendekeza uchunguzi zaidi ufanywe ili kulinda kizazi cha sasa na kijacho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live