Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti kufanyika usugu wa antibayotiki

11704 Dawa+pic TanzaniaWeb

Wed, 18 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Kituo cha utafiti wa tiba Kilimanjaro (KCRI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha St. Andrews cha Uingereza kimeanza utafiti kubaini matatizo yanayosababishwa na usugu wa dawa za antibayotiki zinazotumika kuua bakteria.

Mkurugenzi wa uhakiki ubora wa huduma za afya katika Wizara ya Afya, Dk Mohamed Ally Mohamed amesema nchi za Afrika Mashariki na dunia kwa jumla zinakabiliwa na changamoto ya usugu wa dawa.

Ametaja sababu zinazochangia kuongezeka kwa usugu wa dawa kuwa ni baadhi ya wagonjwa kuzitumia bila kufuata masharti ya madaktari; madaktari kuwaandikia wagonjwa dawa nyingi bila kufuata mwongozo na kutumia dawa za wanyama kutibu binadamu.

Mkurugenzi wa kituo cha KCRI ambacho ni sehemu ya Hospitali ya KCMC ya mjini Moshi, Profesa Brandina Mmbaga amesema uzinduzi wa mradi huo uliopewa jina la Hatua unalenga kubaini changamoto zinazoendana na usugu wa dawa za antibayotiki.

Amesema utafiti unalenga kupata matokeo yatakayosaidia kupata ufumbuzi wa kudumu utakaohakikisha jamii inakua salama kiafya.

Profesa Mmbaga amesema utafiti unafanywa katika nchi za Uganda, Kenya na Tanzania na utafanyika katika vituo vya hospitali ya Bugando mkoani Mwanza, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na KCMC.

Mkuu wa utafiti huo, Profesa Mathew Holden amesema utafiti huo utasaidia kufahamu kwa kina changamoto hiyo na kutoa mapendekezo yatakayosaidia nchi hizo kuimarisha afya za watu wake.

Chanzo: mwananchi.co.tz