Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti! Wanaume wenye miaka 35 na zaidi wanazaa watoto njoti, wenye usonji

Mtoto Kichanga.jpeg Utafiti! Wanaume wenye miaka 35 na zaidi wanazaa watoto njoti, wenye usonji

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanaume wanaoamua kuwa wazazi baada ya miaka 35, upo uwezekano wa kuwa na hatari ya watoto wao kuzaliwa kabla ya muda (Njiti) au wenye hali ya usonji (autism), na kwamba mwaka unaposogea mbegu za uzazi za kiume hupungua ubora wake jambo linalohatarisha uwezo wao wa kuendeleza vizazi.

Haya yamebainishwa na tafiti kadhaa zilizofanywa katika miaka ya hivi karibuni, ukiwemo ule uliofanywa na kitivo cha tiba cha Chuo kikuu cha Stanford nchini Marekiani.

Ambapo pia wanaume wenye watoto baada ya umri wa miaka 35, wana uwezekano wa juu zaidi wa watoto wao kuzaliwa wakiwa na uzito wa chini wa mwili, kuwa na kifafa, au kuhitaji kuongezewa hewa ya kupumua muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Daktari Karla Giusti Zacharias, mtaalamu aliyebobea katika masuala ya uzazi wa binadamu na mjumbe timu ya tiba katika Rede D'Or - São Luiz Itaim Hospital katika São Paulo, anaelezea kwamba mara kwa mara hupokea wanaume katika ofisi yake ambao wangependa kuwa na watoto . .

"Ninawapokea wagonjwa wenye miaka 50 na ushee ambao wanawaoa wanawake vijana ambao wanataka kupata ujauzito na mara nyingi huwa wanauliza ni zipi hatari za baba mwenye umri mkubwa na huwajibu kwa ujumla, mfumo wa uzazi wa mwanaume hufanya kazi tofauti na ule wa wanawake," amesema Dkt. Zacharias

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa hata wakati wanapofanikiwa kuwa na uwezo wa kutungisha mimba, mtoto mchanga anakuwa katika hatari ya kupata matatizo ya mara kwa mara ya kiafya kuanzia kasoro katika mfumo wa kupumua hadi autism.

 Utafiti uliofanywa mwaka 2018 na Chuo kikuu cha Stanford cha tiba ulibaini kwamba kadri mwanaume anavyoendelea kuwa na umri mkubwa, ndivyo mtoto anavyokuwa na uwezekano wa hatari ya kuzaliwa akiwa na kasoro za kiafya.

Wanaume wenye watoto baada ya umri wa miaka 35, wana uwezekano wa juu zaidi wa watoto wao kuzaliwa wakiwa na uzito wa chini wa mwili, kuwa na kifafa, au kuhitaji kuongezewa hewa ya kupumua muda mfupi baada ya kuzaliwa.

 Watu wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wana uwezekano wa 14% zaidi wa kupata watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda wao kufika na wale wenye zaidi ya umri wa miaka 50 wana uwezekano wa 28% zaidi wa watoto wao wanaozaliwa kuhitaji kuwekwa katika kitengo cha matibabu ya dharura (Intensive care unit) kwa muda.

Katika chapisho hilo hilo Michael Eisenberg, profesa wa masuala ya uzazi na mkuu wa utafiti, anabainisha kwamba idadi hiyo haipaswi kutafriwa kama kitu cha kutisha na kusema matokeo ya utafiti huu yanapaswa kusaidia familia kupanga vyema na kufuatilia afya yao ya uzazi kadri inavyopaswa.

Katika hitimisho, utafiti huo unabainisha kuwa, kwa kila miaka 10 ya ongezeko la umri wa baba, kuna 21% ya fursa ya ziada kwamba mtoto ataugua kutokana na hitilafu, zinazohusiana na ugumu wa kuwasiliana, maingiliano ya kijamii na kitabia.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live