Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utafiti: Dawa bandia tishio kubwa Afrika

Dawa Bandia Feki.jpeg Utafiti: Dawa bandia tishio kubwa Afrika

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dawa bandia, feki au za kughushi ni tatizo kubwa katika nchi nyingi za Afrika. Utafiti unaonyesha kuwa nchi nyingi zinazoendelea zina kiwango kikubwa cha dawa zisizo na viwango.

Kwa mfano, hadi asilimia 88.4% ya dawa za malaria katika baadhi ya masoko ya Afrika zimeripotiwa kuwa bandia. Kutumia dawa zisizo na ufanisi husababisha vifo kati ya 64,000 na 158,000 vinavyohusishwa na ugonjwa wa malaria kila mwaka katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kuwapa watu dawa ambayo haitafanya kazi mwilini au haijatengenezwa vizuri kusaidia ugonjwa husika ni hatari. Zaidi ya watoto 250,000 duniani kote hufa kutokana na dawa feki kila mwaka. Katika mwaka uliopita pekee zaidi ya watoto 300 walikufa baada ya kutumia dawa feki za kikohozi au dawa za maumivu.

Juhudi zinaendelea kuimarisha ufuatiliaji wa serikali kuhusu dawa bandia.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hadi asilimia 50 ya dawa katika eneo la Afrika magharibi hazikidhi vigezo vinavyostahili au ni bandia. Hayo yamo katika ripoti maalumu ya Umoja wa Mataifa kuhusu biashara haramu ya bidhaa za matibabu.

Aidha kwa mujibuu wa Umoja wa Mataifa ni kuwa, kote eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, hadi dola milioni 44.7 zinatumiwa kila mwaka kutibu watu waliotumia dawa bandia za malaria au zisizokidhi vigezo na viwango vinavyostahili.

Mbali na hatari ya bidhaa bandia na dawa zilizotengenezwa vibaya, ambazo hazifanyi kazi kama inavyotakiwa na mbaya zaidi kusababisha maambukizi ya magonjwa hatari, ripoti zinaonya pia kuhusu dawa halali kutumiwa kwa njia zisizoidhinishwa na wataalamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live