Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usisafishe sikio kwa pamba!

Lady Ceaning Her Ears Usisafishe sikio kwa pamba!

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wameshauriwa kutoingiza maji kwenye masikio wakati wa kuoga pia kutosafisha masikio yao kwa kutumia pamba za masikio, kwani kwa kawaida sikio hujisafisha lenyewe.

Hayo yamebainishwa na daktari bingwa wa pua, koo na masikio, Dk Jane Bazilio kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Pwani -Tumbi, wakati wa kambi ya huduma za kibingwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora-Kitete.

Dk Bazilio amesema kwa kawaida sikio huwa linajisafisha lenyewe, hivyo mtu anapotumia pamba anakuwa anatoa nta iliyoko kwenye sikio ambayo kazi yake ni kulilinda sikio.

“Katika kambi hii tumewaona wagonjwa wengi wenye matatizo ya masikio na pua, wananchi wengi wanafikiri ile nta ni uchafu kutokana na rangi yake ile ya kahawia (Brown) na kusema wanatoa uchafu ile sio uchafu ina kazi yake ya kulinda sikio, nta ile msiitoe ina utaratibu wake wa kutoka kwenye sikio,”amesisitiza Dk Bazilio.

Amesema wagonjwa wengi waliowaona katika kambi hiyo, wanakuwa na shida ya fangasi masikioni, ambayo husababishwa na unyevunyevu kwenye masikio na kuwataka wananchi wanapokuwa wanaoga wasiingize maji kwenye masikio yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live