Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushauri wa Ujerumani kuhusu matumizi ya Chanjo za Moderna

Moderna Pic Ujerumani yatoa ushauri matumizi chanjo za Moderna

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya afya nchini Ujerumani imetoa ushauri kuhusu ya chanjo ya Corona aina ya Moderna kwa watu walio chini ya miaka 30 kufuatia kuwepo kwa ushahidi wa kuwa chanjo hiyo inasababisha maradhi ya moyo.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na kituo cha chanjo Stiko zinaonesha kuwa chanjo hiyo inasababisha kuvimba kwa misuli pamoja tishu zinazozunguka moyo.

"Kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 30 hawapo kwenye hii hatari" imesema taarifa hiyo.

Aidha kituo hicho kimetoa mwongozo mpya wa chanjo ya Corona kwa kutoa mapendekezo haya;

"Kwa watu walio na umri chini ya miaka 30 kupewa chanjo aina ya Comirnaty pekee" Taarifa hii imetolewa siku moja mara baada ya kituo cha chanjo cha Ufaransa kutoa mapendekezo kama haya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live