Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upungufu wa nguvu za kiume

55320 Nguvu+za+kiume+pic

Fri, 3 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tatizo la kupungua kwa nguvu za kiume limekuwa likiwakumba wanaume wengi nchini.

Baadhi yao hulazimika kula vipande vya nazi, karanga na muhogo mbichi kwa madai ya kwamba ni tiba mbadala ya tatizo hilo.

Mbali na tiba hizo, wengine hunywa supu ya pweza na vidonge vya hospitalini ili kujitibu.

Yafuatayo ni miongoni mwa mambo yanayosababisha kupungua kwa nguvu za kiume.

Magonjwa

Endapo utakuwa unakabiliwa na magonjwa sehemu za siri, tezi dume, kisukari, presha, figo na ini kutofanya kazi vizuri, unajiweka katika hatari ya kupungukiwa na nguvu za kiume.

Ulevi na sigara

Unywaji wa pombe kupindukia ni adui na haufai kwa afya yako kwa kuwa husababisha kupungua kwa nguvu za kiume.

Kujichua

Kujichua kunaweza kusababisha kupata majipu, michubuko, kutojiamini na wakati mwingine kutovutiwa na wanawake.

Matumizi ya dawa

Hapa kuna dawa za kulevya na za dawa kawaida; ila dawa za presha na kisukari huathiri nguvu za kiume.

Njaa

Haifai mtu kushiriki tendo la ndoa huku ana njaa. Hii inaweza kumsababishia kupoteza nguvu za kiume au kupata ugonjwa wa Henia.

Nguo za kubana

Kwa kawaida nguo za ndani zinazobana au chafu zinasababisha magonjwa ya ngozi kutokana na joto. Hali hiyo huathiri mfumo wa nguvu za kiume.

Tiba mbadala

Ikiwa ni mwathirika wa tatizo la kupungua nguvu za kiume; changanya udi karaha na darufilfili, jauza, tangawizi, karafuu na mkuyati. Vyote viwe unga na ujazo sawa, kula kijiko kimoja kutwa mara tatu kwa siku 15

Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu wa tiba mbadala



Chanzo: mwananchi.co.tz