Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upungufu wa maji mwilini husababisha ukichaa

Ubongoooo Ugonjwa Upungufu wa maji mwilini husababisha ukichaa

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ubongo wa mwanadamu unaundwa na takribani asilimia 85 ya maji ambapo upungufu wa hata asilimia moja hupelekea matatizo makubwa ya hadi asilimia tano ya ufanisi na ukubwa wa ubongo.

Upungufu wa maji mwilini kwa muda mrefu husababusha chembe za ubongo kupungua ukubwa na wingi ambapo tafiti zilizofanywa na 'The Brain and Spine Institute' zinaonesha kuwa upungufu asilimia 2 ya ukubwa wa ujazo wa ubongo hupelekea kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi na mtu kushindwa kupiga hesabu za kawaida.

Mtu mwenye upungufu wa maji kwenye ubongo hupata dalili kama msongo wa mawazo, uchovu mwingi wakati wa mchana, sonona, kukosa usingizi, kukosa umakini, kusahau vitu na ubongo kushindwa kuchanganua mambo.

Kwa wastani mtu mzima hupoteza wakia 80 za maji kwa kutoka jasho, kupumua, mkojo na haja kubwa kwa siku.

Inashauriwa kunywa bilauri moja ya maji kabla ya kufanya mazoezi na kunywa wakati wa kufanya mazoezi yako kikamilifu, na bilauri moja kabla ya kula pamoja na kula matunda na mboga zenye asili ya majimaji (tikiti maji na matango).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live