Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upasuaji wa kwanza bila kufungua kifua wafanyika

Upasuaji Bila Kifua.jpeg Upasuaji wa kwanza bila kufungua kifua wafanyika

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Starcare ya nchini India wamefanya upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI).

Taarifa ya JKCI imesema kuwa upasuaji huo umefanyika katika kambi maalumu ya siku mbili ya matibabu ya moyo inayoendelea JKCI.

Taarifa hiyo umesema kuwa upasuaji huo mdogo wa kubadilisha valvu umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live