Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unywaji soda huzeesha haraka

73516 Soda+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Si rahisi kuamini kwa kuwa ni kinywaji kilichozoeleka karibu kila dunia nzima na anayekikosoa anatakiwa awe na rundo la hoja kushawishi watumiaji kudhibiti unywaji.

Lakini ni dhahiri kwamba soda imekuwa ikihusishwa na magonjwa lukuki; saratani, figo, mifupa, mstuko wa moyo.

Pia, unywaji wa vitu vya sukari pia unasababisha kuwa na unene, kitambi na upungufu wa madini muhimu mwilini. Soda haina lishe muhimu wala faida yoyote mwilini, ndivyo wanavyosema wataalamu.

Orodha hiyo ya athari za unywaji soda pia inahusisha kuzeeka haraka, kwa mujibu wa utafitiki uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard cha Uingereza.

Utafiti huo unaonyesha kuwa unywaji wa soda kwa kiwango kikubwa huongeza kasi ya uzee.

Unaeleza kuwa sumu zilizo kwenye soda zinazeesha mapema. Yaani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama wa miaka 40.

Pia Soma

Advertisement   ?
“Soda inaponyweka inaongeza uzito wa nusu kilo kwa siku, hivyo watu wanaozinywa hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi. Hivyo akinenepa kupita kiasi anasababisha mwili wake kuonekana na maumbile ya uzee,” unaeleza utafiti huo.

Pia, daktari wa kutoka Kenya, Theo Wangata anasema kunywa soda kwa wingi kunaweza kusababisha kisukari.

“Kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi. Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu (insulin resisitance) na hali hii husababisha wewe kupatwa na ugonjwa wa kisukari,”anasema.

Takwimu zinaonyesha kuwa binadamu wa kawaida hunywa vinywaji visivyolewesha, kama soda, chupa 42 kwa mwaka (sawa na gramu 1,638 ya sukari au vijiko 92 vya sukari). Tafiti pia zinaeleza kuwa mtu anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa mwaka.

“Soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula. Madini hayo ni muhimu kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kwenye mwili wa binadamu,” anasema daktari bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Delilah Kimambo.

Anasema soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu, hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.

Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kuua figo,” anasema Dk Kimambo.

Pia, anaeleza soda hupunguza kiwango cha maji mwilini kwa kuwa ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambacho humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo (kidney stone) na mawe kwenye nyongo ya binadamu.

Dk Kimambo anashauri ni vizuri kubadili mfumo wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili kama vile kunywa juisi ya matunda badala ya soda.

Chanzo: mwananchi.co.tz