Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unywaji maziwa washuka nchini

MAZIWA Unywaji maziwa washuka nchini

Mon, 27 Sep 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Imeelezwa kuwa unywaji wa maziwa nchini uko chini ya kiwango cha kimataifa, ambapo Mtanzania mmoja anakadiriwa kunywa lita 50 kwa mwaka ikilinganishwa na kiwango cha lita 200 zinazotakiwa kwa mujibu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP).

Akizungumza na waandishi wa habari lkuhusu maadhimisho ya Siku ya Maziwa duniani, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Anjelina Lutambi, amesema yatafanyika mkoani hapa Septemba 29, 2021 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.

Lutambi amesema kwa kiwango cha unywaji wa maziwa kiko chini hususan katika shule za msingi, ambapo ametoa mfano wa Mkoa wa Kilimanjaro akisema zipo shule 24 zinazotoa maziwa, Mbeya shule nne na Iringa shule mbili, hali aliyosema hairidhishi.

Amesema kwa Tanzani kuna idadi ya shule 210 zenye wanafunzi zaidi 9,000 zenye utaratibu wa kunywa maziwa hivyo kupitia maadhimisho hayo serikali itahamasisha jamii unywaji wa maziwa.

Mfanyabishara wa Maziwa, Tausi Azory amesema kuwa licha ya Serikali kuhamasisha unywaji wa maziwa bado soko la maziwa ni dogo jambo linalochangia bei zake kuporomoka kila kukicha.

Naye Janeth Samson amesema kuwa uwekwe utaratibu wa utoaji elimu kuanzia katika ngazi za familia kuhamasisha unywaji wa maziwa katka ngazi za kata na vijiji.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz