Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unywaji maziwa wapunguza udumavu, utapiamlo Mbeya

Unywajiipic Data Homera akizungumzia takwimu za maziwa mkoani humo

Thu, 7 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema ongezeko la uzalishaji na unywaji maziwa kwa kipindi cha mwaka mmoja umepunguza udumavu na utapiamlo kwa watoto mkoani humo.

Amesema kwa mwaka jana, Mbeya ilikuwa ikizalisha lita 110 milioni, lakini 2022 uzalishaji huo umeongezeka hadi kufikia lita 200 milioni hali iliyopelekea unywaji wa maziwa kupanda mkoani humo.

 “Ni mengi sana Rais wetu katufanyia kwa kipindi cha mwaka mmoja, lakini tunajivunia uzalishaji maziwa kutoka lita milioni 110 na kufikia 150 hadi 200, hali iliyosababisha kuondokana na udumavu na utapiamlo kwa watoto,” amesema Homera.

Naye mdau wa maendeleo mkoani humo, Ndele Mwanselela amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia wawekezaji na wafanyabiashara wameona mabadiliko ikiwamo hali ya ukusanyaji ushuru.

“Hadi sasa tunafurahia uwekezaji tulioufanya hakuna aliyefunga duka au ofisi kwa kudaiwa kodi, TRA wanakusanya mapato kwa utaratibu na hili ni kutokana na mfumo wa kiongozi wa juu,” amesema  Mwanselela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live