Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unyonyeshaji sahihi umetajwa njia ya uzazi wa mpango

NDOAAAAAAAAAA Unyonyeshaji sahihi umetajwa njia ya uzazi wa mpango

Fri, 14 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kaimu Mratibu wa afya ya uzazi mama na mtoto wilayani Shinyanga, Regina Renatus, amebainisha hayo wakati wa utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa akina mama wilayani Shinyanga, pamoja na unyonyeshaji sahihi kwa watoto wadogo walio na umri chini ya miezi sita.

Amesema mama anapokuwa akinyonyesha sahihi mtoto wake, kwa kuzingatia masharti ya unyonyeshaji itamsaidia kutoshika ujauzito, na hatimaye kufanya uzazi wa mpango kwa kuwaachia watoto nafasi, ambapo watakua vizuri pamoja na afya njema.

“Uzazi wa kuacha nafasi una faida nyingi sana, kwanza mzazi atakua na afya nzuri sana, pamoja na mtoto wake, pia ataepukana kwenye hatari ya vifo vitokanavyo na uzazi, sababu via vyake ya uzazi vitakuwa imara, tofauti na yule ambaye ana jifungua watoto mfululizo ambapo kizazi chake hulegea,”amesema Renatus.

Ofisa Lishe Halmashauri wilayani Shinyanga, Said Mankiligo, amesema hali ya unyonyeshaji wilayani humo upo asilimia 65, ambapo matarajio yao hadi kufikia 2025 wafikie asilimia 100.

Nao baadhi ya akina mama wilayani humo ambao wamepata elimu ya afya ya uzazi na unyonyeshaji akiwamo Teresia Bathromeo, mkazi wa kijiji cha Didida, amesema yeye ni miongoni mwa akina mama ambao walikuwa wakikatisha watoto kuwanyonyesha, sababu ya kuwabebea ujauzito wakiwa bado wadogo na kuzaa bila ya kuacha nafasi.

Aidha amesema elimu ya afya ya uzazi na unyonyeshaji ni muhimu sana hasa maeneo ya vijijini, na kuwataka wataalumu wa afya waendelee kuitoa kwa kushirikisha pia na wanaume, ili wafahamu umuhimu wa kuzaa watoto kwa kuacha nafasi.

Chanzo: ippmedia.com