Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unyanyapaa ni hatari kuliko Ukimwi

Unyanyapaa ni hatari kuliko Ukimwi

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania wameomba wawe na mwakilishi wao bungeni atakayekuwa kinara  kuelimisha jamii kuhusu kuwanyanyapaa wenye ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Machi 2, 2020 na mkurugenzi wa taasisi ya wanawake wanaoishi na virusi vya Ukimwi, Joan Chamungu wakati wa maadhimisho ya siku ya kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wenye VVU.

Amesema ubaguzi ni tatizo kubwa linalowafanya wengi wao kupoteza maisha kuliko hata ugonjwa huo.

Amebainisha kuwa kutokana na hali huyo watu wengi wenye virusi wanaishia kujificha na kushindwa kutumia dawa matokeo yake maambukizi yanazidi kuongezeka.

“Tunatamani katika zile nafasi za uteuzi mwenyekiti wa baraza letu la wanaoishi na Ukimwi ateuliwe na yeye kuingia bungeni. Akapaze sauti na jamii ielewe kuhusu athari za unyanyapaa,” amesema Chamungu

Mwenyekiti wa baraza la watu wanaoishi na Ukimwi (Nacopha), Letisia Moris amesema unyanyapaa ni kikwazo kinachokwamisha juhudi za baraza hilo na Serikali katika kuhakikisha watu wanapima afya zao na kuanza kutumia dawa.

Pia Soma

Advertisement
“Unyanyapaa ni tishio kuliko Ukimwi wenyewe, tunanyooshewa vidole na kupewa majina ya ajabu. Tunaomba taasisi za kidini zitusaidie katika kuelimisha jamii,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz