Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unicef yazungumzia jinsi ya kupunguza Nimonia kwa watoto Tanzania

93985 Unicef+pic Unicef yazungumzia jinsi ya kupunguza Nimonia kwa watoto Tanzania

Fri, 31 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (Unicef) limesema kuongeza  juhudi za kupambana na ugonjwa wa Pheumonia (Nimonia) zinaweza kuzuia vifo vya watoto 150,000 nchini Tanzania.

Nimonia ni homa ya mapafu inayoambukiza kwenye mapafu na inayodaiwa kuua watoto wengi hasa katika nchi zinazoendelea.

Kwa mujibu wa taarifa ya Unicef iliyotolewa leo Ijumaa Januari 31, 2020 na Mtaalamu wa Kitengo cha Mawasiliano, Usia Nkhoma uchambuzi kuhusu ugonjwa huo umefanyika katika  mkutano wa kwanza wa dunia unaoendelea mjini Barcelona nchini Hispania kati ya Januari 29-31, 2020.

Kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, hatua za kuzuia maambukizi na kutoa matibabu jumuishi ya ugonjwa huo kunaweza kuokoa maisha ya watoto 61,302 walio chini ya umri wa miaka mitano Tanzania.

Pia, hatua hiyo inaweza kuzuia vifo vya watoto 92,310 vinavyotokana na magonjwa mengine makubwa wakati huohuo.

Unicef inasisitiza kuwepo kwa  huduma za afya jumuishi zinazoweza kutoa matibabu kwa magonjwa yote makubwa kwa watoto kwa wakti huo huo.

Pia Soma

Advertisement

Daktari kutoka Hospitali ya Taaluma na Tiba Mloganzila, Shindo Kilawa anawashauri wazazi au walezi kumpeleka  mtoto hospitalini haraka pindi mtoto anapoonesha dalili za ugonjwa huu badala ya kuamua kumpa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

Dalili za homa ya mapafu kuwa ni kikohozi, maumivu ya kifua, joto jingi mwilini na kushindwa kupumua na husababishwa na maambukizi ya bakteria.

Dk Kilawa anasema maamuzi ya Matibabu kwa watoto wenye homa ya mapafu hutegemea aina ya vimelea, umri na hali ya mtoto.

Hata hivyo anasisitiza kinga zaidi na kuepuka mazingira yanayoweza kusababisha ugonjwa huo kwa watoto.

Chanzo: mwananchi.co.tz