Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unga wa faru hauongezi nguvu za kiume

65612 Faru+pic

Fri, 5 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Kama unadhani unga unaopatikana baada ya kusugua au kusaga pembe ya faru unaongeza nguvu za kiume hakika utakuwa umekosea sana.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Julai 4, 2019 na mratibu wa uhifadhi ya wanyamapori hao nchini Tanzania, Philbert Ngoti katika mkutano wa mwaka wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa) uliowahusisha wahariri na waandishi waandamizi wa habari.

“Kuna uvumi tu ulitokea mji mmoja huko India kuwa unga wa Faru unaongeza nguvu za kiume lakini utafiti ambao umefanyika, imebainika kuwa si kweli,” amesema.

Amesema idadi ya faru imeongezeka nchini baada ya kutoweka kwa asilimia 90 kutokana na kuuawa na majangili.

Chanzo: mwananchi.co.tz