Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unatakiwa kula samaki Kilogramu 20.5 kwa mwaka

SAAAA Unatakiwa kula samaki Kilogramu 20.5 kwa mwaka

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Nazael Madala, amesema wastani wa kila mtu anatakiwa kula Kilogramu 20.5 kwa mwaka lakini kwa Tanzania wastani kwa sasa kwa mtu anakula Kilogramu 8.5 pekee.

Ameeleza hayo alipokuwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki walipotembelea mradi wa shamba la ufugaji samaki uliopo Bagamoyo Mkoani Pwani, ambao utakuwa unazalisha takribani vifaranga Milioni Mbili kwa mwaka na kuuza samaki metriki tani 8,000 hadi 10,000 kwa mwaka.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) akikagua baadhi ya mabwawa ya samaki yaliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Aidha Dkt. Nazael Madala ameongeza kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza kusini mwa janga la sahara kutumia teknolojia hiyo na kwamba watanzania wengi wanaweza kujifunza katika kuongeza tija ya uzalishaji wa samaki kwenye mabwawa.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (kushoto) akikagua baadhi ya mabwawa ya samaki yaliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Waziri Ndaki amesema kupitia shamba la Tanlapia ambalo katika awamu ya kwanza linatarajia kuwa na mabwawa 48 ya samaki, litakuwa shamba darasa la watu kutoka maeneo mbalimbali nchini kujifunza namna ya ufugaji wa samaki kibiashara.  
Chanzo: eatv.tv