Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unapomaliza kumung’unya ubuyu mbegu unatafuna?

81808 UBUYU+PIC Unapomaliza kumung’unya ubuyu mbegu unatafuna?

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hivi huwa unatafuna mbegu za ubuyu au hutafuni? Kama huwa unamung’unya tu bila kutafuna basi unakosa uhondo na faida inayopatikana katika tunda hilo.

Ubuyu ni tunda kama yalivyo matunda mengine, huimarisha kinga ya mwili na mifupa na hapa tunazungumzia ubuyu halisi (fresh) haujachanganywa rangi, ladha wala kitu kingine.

Ofisa lishe wa Mkoa wa Dodoma, Heriet Nyange anasema moja ya faida kubwa iliyopo katika ubuyu halisi una vitamini C nyingi zaidi kuliko matunda jamii ya machungwa na kizuri zaidi huongeza damu mwilini.

“Ubuyu una vitamini C nyingi, mara tano ya ile inayopatikana katika matunda jamii ya machungwa,” anasema Nyange.

Anasema mbali na vitamini C, ubuyu una vitamini A, E, B2 pamoja madini ya chuma, calcium, magnesium, potasium, folic, zinki na protini.

“ Tunda hili pia lina wanga, hivyo raha ya kula ubuyu utafune na mbegu zake na ule ubuyu ambao ni halisi, yaani haujawekwa rangi wala ladha.”

Pia Soma

Advertisement
Anazitaja faida za ubuyu mwilini huimarisha kinga ya mwili, huimarisha afya ya mifupa, husaidia katika mfumo wa umeng’enyaji na huongeza damu mwilini.

Huondoa tatizo la kukosa choo kutokana na kwamba ubuyu una nyuzi nyuzi ambazo husaidia kurekebisha matatizo ya umeng’enywaji wa chakula.

“ Faida nyingine huondoa sumu na mafuta mwili.”

Nyange anabainisha kuwa hata majani ya ubuyu hutumika kama mboga kwa jamii ya Wagogo.

“ Huchuma majani ya ubuyu yale malaini na kuyapika, hivyo kupata mboga aina ya mlenda,” anasema.

Kuhusu watoto wenye umri wa miezi sita na kuendelea, mtaalamu huyo wa lishe anasema wanaweza kuchanganyiwa kidogo juisi ya ubuyu katika uji ili wapate vitamini C na virutubisho vingine.

Makala haya yameandikwa na mwandishi wa gazeti hili.

Chanzo: mwananchi.co.tz