Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unajua kilichomo kwenye maziwa mtindi?

73513 Mtindi+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Je, una tatizo la kuishiwa nguvu za mwili mara kwa mara? Kama ndiyo, basi maziwa mgando au wengi hupenda kuita mtindi yatakufaa.

Katika makala haya nitazungumzia faida za maziwa mtindi katika mwili wa binadamu. Maziwa ni kinywaji na chakula kwa watoto wadogo, watu wazima na wagonjwa.

Hata hivyo, maziwa ni mojawapo ya vyakula vichache ambavyo ni mlo kamili, hiyo ni kwa sababu ya ubora wake wa virutubishi vilivyomo.

Mtindi husaidia kuongeza nguvu mwili, hivyo mtindi ni mzuri kwa watu wenye matatizo ya kuishiwa nguvu mwilini mara kwa mara.

Kaimu mkurugenzi, idara ya sayansi ya chakula ya Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dk Elifatio Towo anavitaja virutubisho hivyo kuwa ni utomwili, kabohaidreti , mafuta , madini na vitamini.

Dk Towo anasema maziwa yaliyochachushwa (mgando/mtindi) ni yale ambayo yameongezwa bakteria wazuri au wanaoweza kuwa tayari kwenye maziwa au katika chombo cha kuchachushia.

Pia Soma

Advertisement   ?
“Bakteria hawa wazuri wanasaidia kubadilisha sukari iliyoko kwenye maziwa freshi kuwa kwenye hali ya uchachu (asidi),” anasema Dk Towo.

Mtaalamu huyo anasema maziwa yaliyochachushwa (mtindi/mgando) yanaorodheshwa kuwa ni miongoni mwa vyakula bora na muhimu katika afya ya binadamu kwa sababu ya kuwa na virutubisho vingi venye faida nyingi katika mwili wa binadamu.

“Baadhi ya virutubisho vinavyopatikana katika maziwa ya mtindi ni pamoja na madini mfano ‘Potassium, Iodine, ‘Phosphorus’ ‘Zinc na Calcium” anasema.

Pia, anabainisha kuwa mtindi una vitamini ‘riboflavin (vitamin B2), na ‘vitamin B12. Anafafanua kuwa wakati wa uchachushaji kuna vichocheo vingine vinavyojulikana kama antioksidants, hivi ndivyo vinavyokinga mwili dhidi ya magonjwa ya kuharisha na aina mbalimbali za saratani.

Chanzo: mwananchi.co.tz