Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy asikitishwa na wasiochanjwa

Chanjo Kugomewa Ummy asikitishwa na wasiochanjwa

Wed, 23 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza kutoridhishwa kwake na idadi ya watu waliojitokeza kupata chanjo ya Uviko 19 hadi sasa ambapo licha ya kuwa na shehena kubwa ya chanjo nchini waliochanjwa ni asilimia 9.8 pekee ya walengwa.

Ameeleza kuwa kwa sasa chanjo ndiyo njia pekee ya kisayansi iliyothibitishwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akipokea dozi  milioni moja kati ya 4 milioni za chanjo aina ya Sinovac kutoka serikali ya Uturuki.

Dozi hizo zinafanya jumla ya dozi 10,845,774 zilizopokelewa hadi sasa nchini huku kukiwa na watanzania 3,016,551 pekee waliochanjwa.

“Chanjo zipo za kutosha tofauti na wenzetu wa nchi jirani, Tanzania zipo chanjo za kutosha watu ndiyo hawajitokezi kuchanja, nitumie fursa hii kuwasisitiza watanzania tuchenje.

“Sasa hivi tunakuja na mpango wa kuzidi kuwafuata wananchi waliko na kuwahamasisha kuchanja wakiridhia tunawachanja, iwe masokoni au hata kwenye vituo vya daladala,” amesema Ummy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live