Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy ashiriki mkutano wa 150 bodi ya WHO

9ad8bc63296b4bf6b66f4b2623752642 Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameshiriki Mkutano wa 150 wa Bodi Tendaji ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ulioanza Januari 24 na kumalizika leo Januari 29 2022 kwa njia ya mtandao.

Washiriki wengine ni Wizara ya Afya kutoka Tanzania bara na Visiwani , Ofisi ya Rais TAMISEMI, pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi.

Tanzania imewasilisha jumla ya maandiko 9 katika ajenda 8 za mkutano huo huku maeneo yaliyoandaliwa ni afya ya mama, mtoto na lishe, magonjwa yasiyoambukiza, kifua kikuu, Ukimwi, magonjwa ya via vya uzazi na ngono, homa ya Ini, mafua makali ya influenza, polio na chanjo.

Waziri Ummy aliwasilisha andiko la afya ya kinywa na meno ambapo alitoa mwelekeo na mikakati ambayo Tanzania imejiwekea kuimarisha huduma katika eneo hilo. Aidha, maandiko mengine yaliwasilishwa na wataalam mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.a

Chanzo: www.tanzaniaweb.live