Tue, 5 Sep 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Tukio hilo limeshuhudiwa pia na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt Godwin Mollel na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe.
Waziri Ummy amemtaka Dkt. Jingu kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya watendaji ndani ya Sekta ya Afya ili kuweza kutekeleza vyema mipango na afua mbalimbali zinazolenga kuboresha ubora wa huduma za afya na kufanya mambo yenye tija kwa wananchi.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live