Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy akemea uhuni matibabu ya malaria

Utafiti: Ugunduzi Wa Bahati Utakavyosaidia Kupambana Na Malaria Ummy akemea uhuni matibabu ya malaria

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka wananchi kote nchini kuhakikisha wanatibiwa bure ugonjwa wa malaria na wasikubali kulipa fedha yoyote kupata vipimo, matibabu ikiwemo dawa au sindano.

Amesema kumekuwa na uhuni unaendelea katika vituo vya afya huku akisisitiza kuwa matibabu yote ya ugonjwa wa Malaria yanatolewa bure kwakuwa dawa zake zipo katika miradi misonge.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Jumatano, Agosti 9, 2023 akiwa Temeke wakati akiendelea na ziara yake ya kutatua changamoto ya ufinyu wa maeneo unaozikabili hospitali na vituo vya afya mkoa wa Dar es Salaam.

"Wataalamu waache uhuni, dawa za Malaria zinapaswa kutolewa bure, bila malipo yoyote hii naisema wazi na wananchi wengi hawatambui hili, kuanzia kipimo cha haraka cha malaria, sindano ya Malaria kali na hata dawa ni za miradi misonge," amesema Waziri Ummy.

Amesisitiza kuwa pia kuna dawa za watoto kuwakinga na kuharaka kundi lingine ni chanjo za watoto ambavyo hivyo vyote vinatolewa bure bila malipo yoyote.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka viongozi wa ngazi za Halmashauri na menejimenti za hospitali kuhakikisha suala la upatikanaji wa dawa linakua la uhakika.

"Tunataka wananchi wapate dawa ndani ya vituo, makundi ya dawa yote yawepo, miondombinu tumejenga na vifaa tumenunua lakini siasa kubwa sasa ni dawa na changamoto ni dawa," amesema Waziri Ummy.

Akizungumza awali, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dk Boniface Mruma amesema upatikanaji wa dawa kwa sasa umefikia asilimia 96 na kwamba kwa mwaka 2022/23 Halmashauri ilipokea ruzuku ya jumla ya Sh550 milioni fedha kwa ajili dawa na vifaatiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live