Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy: Uzembe vituo vya afya haukubaliki

LISHE NA UMMY Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Mama Samia ameshanielekeza tunakwenda kuboresha huduma kwenye Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa na Hospitali za Halmshauri ili Mtu akija Muhimbili aje na jambo ambalo limeshindikana kule chini, tumeona hapa Hospitali za Mwananyamala na Temeke zinaleta Wagonjwa Muhimbili eti kwasababu hawana damu huo ni uzembe hatuwezi kuukubali"

"Muhimbili mnafanya kazi nzuri lakini tumemsikia Zuhura hapa haiwezekani tangu December hadi leo Mtu anapigwa danadana hapati huduma , nimepokea maoni Wananchi wananiambia Waziri..., nimemuona Mtu kanitumia picha mdomo umevimba anambiwa hakuna kitanda na huyo Mtu anakula panadol kila siku"

"Hii naona ni hiyo kuzidiwa na wagonjwa ni lazima tulitatue haikubali Mgonjwa anakuja muhimbili anasubiri miezi miwili, wiki tatu, wiki nne, wiki tano, ili aambiwe hakuna huduma vitanda vimejaa hapa ni lazima tuufumue mfumo mzima wa huduma Muhimbili" ——— Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akiwa Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam leo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live