Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy Mwalimu asema kelele chanzo magonjwa yasiyoambukiza

84361 Kelele+pic Ummy Mwalimu asema kelele chanzo magonjwa yasiyoambukiza

Fri, 15 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu amesema kelele kupita kiasi ni kati ya vyanzo vya kupata magonjwa yasiyoambukiza, kuwataka wananchi kuepukana nazo.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Novemba 14, 2019 mjini Dodoma katika uzinduzi wa mpango wa Taifa wa kuzuia na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Ametaja baadhi ya sababu nyingine za kupata magonjwa yasiyoambukiza ni kutozingatia lishe bora, mazingira, matumizi ya chumvi nyingi pamoja na sukari.

Amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa watu milioni 41 sawa na asilimia 71 ya vifo vinavyotokea duniani hutokana na magonjwa hayo.

Amebainisha kuwa takwimu zinaonyesha Tanzania vifo vitokanavyo na magonjwa hayo vimeongezeka kwa asilimia  6 katika kipindi cha miaka miwili kutoka asilimia 27 mwaka 2015 hadi asilimia 33 mwaka 2017.

Chanzo: mwananchi.co.tz