Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy Mwalimu aingilia kati gharama za hoteli kwa walio karantini

100189 Ummy+pic Ummy Mwalimu aingilia kati gharama za hoteli kwa walio karantini

Thu, 26 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Afya Tanzania, Ummy Mwalimu amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kubainisha hoteli za gharama ndogo ili wanaoingia nchini kutoka nchi zenye maambukizi ya virusi vya corona waweze kumudu na kukaa karantini kwa siku 14.

Ametoa maelezo hayo baada kuibuka malalamiko ya baadhi ya wageni kuwa wanapelekwa kwenye hoteli zenye bei kubwa hali inayosababisha kushindwa kumudu gharama.

Leo Jumanne Machi 24, 2020 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter,  Ummy amesema, “tumepokea hii changamoto ya sehemu zilizobainishwa kwa ajili ya siku 14 za wasafiri  waliotoka nchi zilizoathirika zaidi na virusi vya corona kukaa. Nawaelekeza ma RC na RAS wa Mikoa yote kubainisha hoteli na sehemu ambazo wasafiri wengi watamudu gharama.”

Chanzo: mwananchi.co.tz