Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy: Mtu mmoja anakunywa pombe lita 10.4, inasikitisha!

Pombe Kibali Ummy: Mtu mmoja anakunywa pombe lita 10.4, inasikitisha!

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema takwimu zinaonesha kuwa wanywaji wa pombe wameongezeka nchini hali inayofanya kuanza uhamasishaji wa kupunguza unywaji wa pombe.

Takwimu alizotoa zinaonesha kuwa mtu mmoja anakunywa lita 10.4 kwa mwaka ambapo awali mtu mmoja alikuwa anakunywa lita 9.1.

Akizungumza katika Mkutano wa Kwanza wa Mipango Mikakati wa Kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza Afrika (ICPPA) Ummy amesema takwimu za mwaka 2016 watu waliokuwa wanakunywa pombe walikuwa asilimia 26 na walipunguza hadi asilimia 20 lakini kiwango cha unywaji pombe kimeongezeka kwa sasa.

“Tunahamasisha kupunguza unywaji wa pombe ulipitiliza tumeongeza kiwango mtu mmoja anakunywa lita 10.4 kwa mwaka hii ni hatari kwa afya,”amesisitiza ummy Ummy amesema kuwa Tanzania kama nchi zingine inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kudhibiti na wanaona ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa yasiyoambukiza husani shinizo la juu la damu,kisukari,masuala ya afya ya akili,selimundu na mengine ikiwemo ajali.

“Tutaendelea kuwekeza katika mikakati ya kinga na kuhakikisha wananchi wanapata huduma na kwenye kinga tutajikita katika kutoa elimu ya afya kwa wananchi kujikinga na tumekuwa na wataalamu kama Prof Janabi wamekuwa wakihamasisha kuzingatia ulaji unaofaa.

Aidha amewasisitiza vijana kufanya mazeozi na wasisubiri wapate magonjwa hayo ndio waanze kufanya mazoezi. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live