Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, ameweka wazi mchakato mpya wa usajili wa wanachama katika mfumo wa bima ya afya, ambapo waajiri watalazimika kuwasajili waajiriwa wao ndani ya siku 30 tangu kuanza kwa mkataba wa ajira.
Waziri huyo, amesisitiza kuwa kila mtu katika sekta rasmi na isiyo rasmi atalazimika kujiunga na "Scheme" ya bima ya afya.
Aidha kwa kuwa kifungu cha 21 katika sheria hiyo ya bima ya afya kwa watu wote kinaweka kiwango cha mchango wa wanachama kutoka sekata hizo, Waziri amependekeza marekebisho kwa kifungu hicho, ambapo ametaka mwajili kuchangia asilimia sita ya mshahara wa mfanyakazi wake.
Hata hivyo, Waziri Ummy amesisitiza kuwa sekta binafsi hailazimishwi kusajili waajiriwa wao katika mfuko wa umma, na badala yake wanaweza kuchagua kusajiliwa katika mifumo binafsi, lakini ni sharti wawe na bima ya afya kama sheria inavyotaka.