Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy: Hakuna mgonjwa mpya wa Marburg

Ummy: Wenyeviti Mabaraza Na Bodi Za Kitaaluma Simamieni Maadili Ummy: Hakuna mgonjwa mpya wa Marburg

Sun, 26 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia leo tarehe 25 Machi, 2023 hakuna Wagonjwa wapya wa Marburg walioripotiwa licha ya kupokea tetesi sehemu mbalimbali Mkoani Kagera.

Ummy akiwa Mkoani Geita amesema ugonjwa huo unaendelea kudhibitiwa ambapo ameambatana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani Dkt. Zabron Yoti na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNICEF, Shalini Bahuguna

“Tangu kuanza kwa ugonjwa huu hadi leo tumeendelea kuwa na jumla ya Wgonjwa walewale nane waliothibitika ambapo watano kati yao walifariki na Watatu wanaendelea na matibabu katika vituo vya kutolea huduma vilivyoainishwa.”

Aidha, Ummy amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Wadau mbalimbali inaendelea kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu kwa kutekeleza mikakati mbalimbali.

“Miongoni mwa hatua ni kuwaweka sehemu maalumu Watu wote waliohudumia Wagonjwa ambao ni Wanafamilia waliouguza Wagonwja na Watumshi wa Afya waliohudumia Wagonjwa, kwa siku 21 ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu kama watabainika na maambukizi.”

Katika kuendelea kudhibiti ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya imeongeza Wataalamu 6 wa afya ikiwemo Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Figo, Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani na Wauguzi waliopata mafunzo maalumu kutoka maeneo mengine ili kusaidiana na Wataalamu wa Afya Mkoani Kagera.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live