Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukikutana na taarifa hizi kuhusu corona, zipuuze

99718 Pic+corona Ukikutana na taarifa hizi kuhusu corona, zipuuze

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Katika kipindi hiki ambacho maambukizi ya virusi vya corona yamezidi kuenea ulimwenguni kote ikiwamo Tanzania, kuna taarifa nyingi rasmi kuhusu tiba ya virusi hivyo.

Watu wamekuwa wakishauriwa kufanya baadhi ya mambo ambayo si sahihi wakiaminishwa kuwa yanazuia au kutibu ugonjwa huo.

Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya afya wamebainisha kwamba kuna taarifa nyingi za upotoshaji kuhusu kutibu au kuzuia ugonjwa wa corona.

Taarifa hizo zisizo sahihi zimekuwa zikisambaa kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram, Facebook na Whatsapp na kuwaweka wananchi njiapanda wasijue kipi cha kweli na kipi cha uongo.

Kutokana na hali hiyo, Dk Li Ping anayeshughulikia magonjwa yanayoambukiza katika hospitali ya Nanjing, China anataja baadhi ya taarifa za uvumi au upotoshoji zilizosambaa kuhusu corona, na jinsi ambavyo njia hizo haziwezi kukabiliana na virusi hivyo.

Uvumi wa kwanza ni kwamba kunywa maji ya moto kunaweza kuua virusi vya corona.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Dk Ping anasema ukweli ni kwamba maji ya moto yanapita kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wakati virusi viko kwenye mfumo wa upumuaji, mifumo ambayo ni tofauti.

Uvumi wa pili ni kwamba vitamini C inaweza kuboresha kinga ya mwili kukabiliana na corona.

Mtaalamu huyo anabainisha kwamba vitamin C inaweza kusaidi kazi za kawaida za kinga ya mwili lakini haiwezi kuongeza kinga dhidi ya virusi vya corona na wala haina athari zozote kwa virusi hivyo.

Uvumi wa tatu ni kwamba kuvaa barakoa (masks) nyingi kunaweza kuzuia virusi vya corona.

Dk Ping anasema virusi vya corona huambukizwa kwa njia ya majimaji na siyo lazima kuvaa barakoa (mask) ili kuvuzia.

Uvumi wa nne kuwa ni wanyama wafugwao wanaweza kueneza virusi vya corona.

Lakini Dk Ping anasema usahihi katika uvumi huu ni kwamba hakuna ushahidi kwamba wanyama wafugwao kama mbwa na paka wanaweza kueneza virusi hivyo.

Uvumi wa tano ni kutumia dawa za kuua bakteria inaweza kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Dk Ping anabainisha kwamba dawa za kuua bakteria zimewekwa kwa ajili ya kuua bakteria na zikitumika kuua virusi zitafanya upinzani wa bacteria kuwa mbaya zaidi.

Tahadhari zinazopendekezwa

Dk Ping anabainisha njia tano za tahadhari dhidi ya virusi vya corona; kwanza, ni kunawa mikono kwa sabuni au kemikali iliyotiwa ethano kwenye maji ya yanayotiririka.

Anasema kugusa shavu baada ya kugusa kitu kilichochafuliwa, kunamuweka mtu katika hatari zaidi.

Pili, anasema acha madirisha wazi ili kuruhusu hewa kuingia ndani.

Pia, anashauri watu kutumia dawa za kuua wadudu mara kwa mara na kusafisha vitu vya ndani kama vile meza za jikoni, viti na madawati.

Anasema ikiwa unakohoa au kupiga chafya, funika mdomo wako kwa kitambaa au karatasi na baada ya hapo tupa karatasi au kitambaa hicho kwenye pipa la takataka lililofunikwa na kisha osha mikono yako kwa sabuni.

Dk Ping anasema inapendekezwa pia kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu na epuka kwenda sehemu zenye mkusanyiko mkubwa wa watu au maeneo unayoweza kugusana na wagonjwa. Anabainisha kuwa endapo mlipuko utatokea, vaa barakoa (mask) wakati wa kwenda nje.

Chanzo: mwananchi.co.tz