Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujumbe wa Butiku kuhusu corona

102409 Butku+pic Ujumbe wa Butiku kuhusu corona

Tue, 14 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amewataka watanzania kuzingatia maagizo na mapendekezo yanayotolewa na Serikali ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa kuwa havichagui Mkristo wala Muislamu.

Butiku alitoa wito huo juzi wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam kuhusiana na hali ya maambukizi ya virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa covid 19.

“Ugonjwa huu hauchagui Mkristo wala Muislamu natoa mapendekezo kama mzee tuzingatie maagizo na mapendekezo bila kushindana na Serikali kwa imani zetu,” alisema.

Alisema dini si ushirikina, bali ni imani na kueleza kuwa kwa Wakristo kanisa lipo ndani yao na si kwenye jengo, hivyo katika hali hii si vizuri kuwa na ubaguzi wowote bali kuzingatia maagizo.

“Ugonjwa huu ukiuona matokeo yake ni zaidi ya vita. Ni ugonjwa unaopiganisha wanadamu na uwezo wao wote. Unaona Marekani wana uwezo mkubwa lakini wanahangaika, China nao wanahangaika, lakini Burundi wenye uwezo mdogo Mungu anawalinda,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo ni vema viongozi wangekuwa na mkakati wa pamoja wa kushughulikia tatizo hilo.

Pia Soma

Advertisement
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Waziri wa afya, Ummy Mwalimu ilieleza kuwa idadi ya watu walioambukizwa na virusi hivyo imefikia watu 49 baada ya kubainika wagonjwa wapya 17.

Kati ya wagonjwa hao 14 ni kutoka Tanzania Bara, 13 wakitokea Dar es Salaam na mmoja Arusha, huku Zanzibar wagonjwa wapya wakiwa watatu.

Alisema wagonjwa hao wanaendelea kupatiwa matibabu na wamewekwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa wataalamu wa afya.

Chanzo: mwananchi.co.tz