Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujenzi viwanda vya dawa kupunguza gharama

Pharmacy Duka La Dawa Ujenzi viwanda vya dawa kupunguza gharama

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema Serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda vya dawa lakini kwa kuwa uamuzi huo ni wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hakuna atakayefanikiwa kuvikwamisha, hivyo vitajengwa.

Amesema kwa sasa serikali inaagiza dawa kwa asilimia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 kutoka nje ya nchi, hali inayosababisha uhaba wa vifaa na gharama kubwa za uagizaji wa vifaa vya afya hivyo ni lazima kuchukua maamuzi magumu.

Dkt. Mpango amezungumza hayo mkoani Njombe wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha mipira ya mikono (Gloves) kinachosimamiwa na Bohari ya Dawa (MSD).

“Tumeamua kuipatia MSD majukumu ambayo ni uzalisha, ununuzi, utunzaji niwahakikishie viwanda hivi vitajengwa," amesema Dkt. Mpango akiongeza kuwa wapo katika mkakati wa kuiongezea mtaji MSD ili kujenga viwanda na maghala na kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

Naye Naibu Waziri wa Afya Dkt.Godwin Mollel amesema, wizara inatambua mapinduzi makubwa yanayofanywa na na Serikali yake katika kuleta mapinduzi sekta ya viwanda hususani vya dawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live